Rais mpya wa nchi ya Burundi Evariste Ndayishimiye ameapishwa leo Juni 18, 2020 katika sherehe zilizohuzuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Katika msafara wa ujumbe wa Tanzania, Mama Samia aliongozana pia na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Evariste Ndayishimiye, ambaye alishinda uchaguzi mwezi uliopita alitarajia kuanza majukumu yake mnamo 20 mwezi Agosti. Ameapishwa miezi miwili kabla kutokana na kifo cha ghafla cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunzinza aliyefariki dunia tarehe 9 Juni baada ya kupatwa na mshituko wa moyo.
Mhe. Ndayishimiye amepishwa kuanza rasmi muhula wake wa miaka 7, katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 Mei, 2020 alipata asilimia 68.72 ya kura huku mpinzani wake Agathon Rwasa akipata asilimia 24.19.
Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayishimiye akiapa ili kuanza kuiongoza Burundi.
Rais mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akikagua gwaride baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi Juni 18, 2020 katika uwanja wa Ingoma mjini Gitega nchini Burundi, hafla iliyohudhuriwa pia na Makamu ya Rais wa Tanzanina Mhe. Samia Suluhu.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi Gasten Sindimwo alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bujumbura nchini Burundi kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye shughuli ya kuapishwa Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayishimiye.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.