HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo wamefanya operesheni ya kudhibiti Ndege waharibifu wa mazao kwa mara ya pili katika eneo la Chigongwe Jijini humo ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kuwa mazao ya wakulima hayaharibiwi na kusababisha upungufu wa chakula.
Zoezi hili limefanyika kwa kutumia Ndege maalum ya kunyunyizia dawa ili kupunguza athari za ndege hao kwenye mazao zinazoweza kusababisha kupungua kwa usalama wa Chakula ambapo hatua hii imechukuliwa baada ya ndege wanaokadiriwa kufikia 1,200,000 kuonekana katika maeneo ya kata ya Zuzu, Chigongwe na mtaa wa Kitelela katika kata ya Miyuji.
Akizungumzia madhara yanayoweza kusababishwa na makundi hayo ya ndege, Afisa Kilimo na Ushirika wa Jiji la Dodoma Yustina Munishi alisema ndege hao, mmoja anaweza kula gramu 5 kwa siku, hivyo kwa idadi ya Ndege walioonekana wanaweza kula gramu 42,000,000 au kilo 42,000 ndani ya siku saba, hivyo endapo makundi haya ya ndege yasipodhibitiwa mapema, yanaweza kuleta uharibifu na hasara kubwa kwa wananchi.
Alisema pamoja na eperesheni hiyo kufanywa, bado wataalam wa Kilimo wa Jiji wanaendelea kufanya ufuatiliaji ili kuona na kujiridhisha endapo tatizo la Ndege hao waharibifu litakuwa limeisha .
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.