• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ndejembi akemea tabia ya wizi kwa watumishi wa Umma

Imewekwa tarehe: December 15th, 2022

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amekemea tabia ya baadhi ya watumishi wa umma nchini kujihusisha na vitendo vya wizi ambavyo vinakwenda kinyume na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuujenga Utumishi wa Umma wenye uadilifu na unaowajibika kwa wananchi kwa kutoa huduma bora.

Akizungumza na Watumishi wa Umma wa Wilaya ya Ilala, Ndejembi amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ana maono makubwa ya kuujenga utumishi wa umma wenye uadilifu, hivyo amewataka watumishi wa umma nchini kutokumuangusha badala yake wafanye kazi kwa bidii na uadilifu mkubwa katika kulitumikia taifa.

“Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua wazi kututhamini watumishi wa umma kwa kuboresha maslahi na stahili zetu hivyo, hatuna budi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuunga mkono kwa vitendo dhamira yake ya kuujenga Utumishi wa Umma wenye uadilifu na unaowajibika kwa wananchi,” Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma kutafakari madhara ya wizi na kutathmini mienendo yao ili kutokuwa ni sehemu ya kukwamisha dhamira ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha huduma kwa wananchi na kuliletea taifa maendeleo katika sekta zote muhimu kama vile afya, kilimo, uvuvi, biashara, uwekezaji na miundombinu.

Sanjari na hilo, Ndejembi amewataka Waajiri na Maafisa Utumishi Serikalini kuwasimamia vema watumishi wanaowaongoza badala ya kusubiria mpaka viongozi wa juu wa kitaifa kufika katika maeneo yao ya kazi kukemea uovu pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.

Akizungumzia matumizi ya fedha za umma, Ndejembi amesema kuwa fedha za umma zinapaswa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali kwani kinyume na hilo ni ukosefu wa maadili katika Utumishi wa Umma.

Ndejembi ameeleza bayana kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita haitomvumilia mtumishi yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma kwa kujihusisha na vitendo vya wizi katika eneo lake la kazi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ndejembi ameendelea na ziara ya kikazi Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.