TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuelekea Uchaguzi wa Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba mwaka huu imefanya kikao na Vyama vya Siasa kilichofanyika tarehe 01 Agosti, 2020 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Semistocles S. Kaijage katika hotuba yake amesema kuwa Tume imefanya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu ya Wapiga kura mara mbili. Katika awamu zote mbili za uboreshaji, jumla ya Wapiga Kura wapya 7,326,552 waliandikishwa sawa na asilimia 31.63 ya Wapiga Kura 23,161,440 walioandikishwa mwaka 2015.
Aidha, jumla ya Wapiga Kura 3,548,846 waliboresha taarifa zao na Wapiga Kura 30,487 waliondolewa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutokana na kukosa sifa kwa mujibu wa sheria. Baada ya kutoa Wapiga Kura ambao taarifa zao zimejirudia, Daftari kwa hivi sasa lina jumla ya Wapiga Kura wapatao 29,188,347 (Milioni ishirini na tisa laki moja themanini na nane, mia tatu arobaini na saba) tu.
Kutokana na idadi hiyo wa Wapiga Kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutakuwa na vituo 80,155 ya kupigia kura na kila kituo kimoja kitakuwa na Wapiga Kura wasiozidi 500.
Bofya hapa kusoma hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa: HOTUBA YA MWENYEKITI - NEC
Chanzo: tumeyauchaguzi_tanzania (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.