• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

NEC yawataka wasimamizi wa uchaguzi kuwepo ofisini muda wote kesho Agosti, 25

Imewekwa tarehe: August 24th, 2020

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kuwepo kwenye ofisi zao kesho wakati wote wa kupokea fomu za uteuzi kutoka kwa wagombea ubunge na udiwani kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na iwapo hawatakuwepo ofisini kwa muda huo Tume itachukua hatua kali dhidi yao.

Hayo yamesemwa leo tarehe 24 Agosti mwaka 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa (Mst.) Semistocles Kaijage wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya kupokea fomu za uteuzi na uteuzi wa wagombea kesho tarehe 25 Agosti 2020.

Jaji Kaijage alisema kesho tarehe 25 Agosti, 2020, Tume itafanya uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge na madiwani nchi nzima.

Alisema uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais utafanyika katika ofisi za Tume zilizopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma na uteuzi wa wagombea ubunge utafanyika katika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo na udiwani katika ofisi za wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata.

“Hadi hivi leo, wagombea wa vyama vya siasa 17 vyenye usajili wa kudumu wamechukua fomu za uteuzi wa kiti cha Rais na makamu wa Rais. Kwa upande wa ubunge na udiwani, Tume inaendelea kukusanya taarifa za waliochukua fomu baada ya kupendekezwa na vyama vya siasa.” amesema Jaji Kaijage.

Alifafanua kuwa kesho tarehe 25 Agosti, 2020 ndiyo siku ya uteuzi na kwamba baada ya zoezi la uteuzi, fomu zitabandikwa katika mbao za matangazo za ofisi iliyohusika na uteuzi.

Jaji Kaijage alisema kwa mujibu wa kanuni ya 29 ya kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 na kanuni ya 27 ya kanuni za Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2020, fomu hizo zitawekwa eneo la wazi hadi saa 10 kamili jioni tarehe 26 Agosti, 2020, ambapo wagombea watapata nafasi ya kuweka pingamizi.

Aliongeza kuwa wengine wanaoruhusiwa kuweka pingamizi ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msajili wa Vyama vya Siasa.

“Tume inaelekeza na inawasisitiza Wasimamizi wa Uchaguzi wa majimbo na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata kuwepo kwenye Ofisi zao kesho wakati wote kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. Kitendo cha kutokuwepo ofisini katika muda huo kitapelekea Tume kuchukua hatua kali dhidi ya watendaji wa majimbo na kata husika.”amesisitiza Jaji Kaijage.

Kwa upande wa kampeni za uchaguzi, Jaji Kaijage alisema kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi kampeni za uchaguzi zinatarajiwa kuanza tarehe 26 Agosti, 2020 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni tarehe 27 Oktoba 2020, ikiwa ni siku moja kabla ya Siku ya uchaguzi yaani tarehe 28 Agosti 2020.

Alisema kwa upande wa Tanzania Zanzibar, kampeni zitahitimishwa tarehe 26 Oktoba, 2020 ili kupisha upigaji kura wa awali na kwamba Tume inawakumbusha wahusika wa Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kutii, kuheshimu na kuzingatia Maadili, Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa, yakiwemo makatazo mbalimbali yaliyomo katika Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2020.

Jaji Kaijage alivikumbusha vyama vya siasa kuzingatia maelekezo yaliyomo katika Maadili ya Uchaguzi hasa katika eneo la kuzitumia kamati za maadili kutatua migogoro na malalamiko yatakayojitokeza.

Alisema Tume kwa upande wake itaendelea kuzingatia Katiba, Sheria, kanuni za uchaguzi na maelekezo yaliyomo katika Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2020.

Chanzo: Tovuti ye NEC (www.nec.go.tz)



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.