Baraza la Mitihani nchini NECTA limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (Darasa la saba) ambapo matokeo yanaonesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.76% tofauti na ufaulu wa 2017 ambao ulikuwa asilimia 72.76%. Dk. Charles Msonde amesema katika tathmini ya awali, kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.9% ikilinganishwa na 2017, amesema pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza uko chini sana tofauti na masomo mengine (-50%).
Aidha, Baraza la Mitihani nchini limewafutia matokeo watahiniwa 357, waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani iliyofanyika mwaka huu 2018.
"Baraza limezuia kutoka matokeo ya watahiniwa zaidi 100 kutokana na kuugua kipindi cha mtihani na kuwapa fursa ya kufanya mtihani huo mwaka 2019" alisema Dk. Charles Msonde.
Kuona matokeo hayo | Fungua link zifuatazo
Matokeo ya Tanzania nzima:
https://www.necta.go.tz/results/2018/psle/psle.htm
Kusoma TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) SEPTEMBA, 2018
Bofya hapa: Taarifa ya matokeo psle 2018.pdf
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.