HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH) ya Jijini Dodoma imetangaza neema kwa Watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo kuwa kutakuwa na Kambi ya Madaktari Bingwa wa Moyo kwa Watoto.
Katika tangazo lao kwenye ukurasa rasmi wa Instagram BMH wameandika kuwa wanayofuraha kuwatangazia Kambi hiyo ambayo watashirikiana na Shirika la The One New Heart Tanzania na Shirika la For Hearts and Souls kutoka Marekani, wataweka kambi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Tangazo hilo limefafanua kuwa Kambi hiyo itaanza leo tarehe 12 mpaka 16 Julai 2021. Huduma mbalimbali zitatolewa ikiwemo upimaji, matibabu ya moyo na operesheni za moyo kwa Watoto.
Hospitali ya Benjamini Mkapa imetoa mwaliko kwa wazazi wote wenye Watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo wawapeleke Watoto hao ili wapate matibabu.
Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa bmhdodoma
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.