Na. Sizah Kangalawe – Habari, Dodoma RS
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayotekeleza shughuli zake mkoani Dodoma yametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji ili kuhakikisha yanatoa mchango chanya kwa maendeleo ya jamii bila kukiuka misingi ya utawala bora. Wito huo umetolewa katika mkutano wa mashirika hayo, uliofanyika Jijini Dodoma Julai 23, 2025.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Msaidizi, Seksheni ya Viwanda na Uwekezaji, Bi. Mwajabu Nyamkomora, alipomuwakilisha RC Rosemary Senyamule katika ufunguzi wa mkutano wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Dear Mama jijini Dodoma.
"Ofisi ya Mkuu wa Mkoa isingependa kupokea malalamiko ya ukiukwaji wa sheria na kanuni unaofanywa na baadhi ya mashirika, badala ya kuhakikisha jamii inapata maendeleo yaliyokusudiwa.
"Nitumie fursa hii kuwakumbusha wote kuwa makini, kuongeza ufanisi na kuepuka migogoro ya aina yoyote ili kuleta maendeleo yaliyokusudiwa."
Hata hivyo, Bi. Nyamkomora ameyataka mashirika hayo kufanya kazi zao kwa uwazi hususan katika vyanzo vyao vya mapato.
"Ninaamini kupitia mkutano huu, tutaweka makubaliano ya utekelezaji wa pamoja na uwazi katika vyanzo vya mapato, aina ya miradi, maudhui ya miradi, na uwajibikaji kwenye mipango yote inayotekelezwa kuanzia ngazi ya vijiji, kata, wilaya hadi mkoa ili kurahisisha kazi ya usimamizi na ufuatiliaji," amesema Nyamkomola.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Mkoa wa Dodoma, Bw. Isaya Silungwe, ameweka bayana mwelekeo wa Taasisi hizo kwa miaka mitano ijayo.
"Mashirika Mkoani Dodoma yameweka vipaumbele ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kiutawala, uwazi na uwajibikaji, kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili kupunguza utegemezi wa wafadhili, pamoja na kuanzisha mfuko wa maendeleo wa kusaidia mashirika yenye changamoto," amebainisha Silungwe.
Naye Msajili wa mashirika hayo Mkoa wa Dodoma, Bi. Honoratha Rwegasira, amesema mkutano huo wa siku mbili, ukijumuisha ushiriki wa mashirika 211, umefanyika kwa ngazi ya mkoa ambapo awali ulitanguliwa na mikutano ya ngazi za wilaya ikiwa ni ku
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.