Wamiliki wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) Jijini Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanatekeleza kwa ufasaha yale yote waliyoyaandika katika mipango kazi yao ya mwaka 2020/2021.
Hayo yalisemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Sharifa Nabalang’anya alipokuwa akizungumza na wamiliki wa mashirika hayo katika kikao maalum cha kuyajengea uwezo mashirika yasiyo ya Kiserikali Jijini hapa.
Sharifa alisema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya mimba za utotoni, ufaulu shuleni pamoja na vitendo vya ukatili kama vile ulawiti na ushoga, vitu ambavyo havileti picha nzuri katika jamii za kitanzania, na wao kama Serikali wanalitambua hilo lakini wakishirikiana na mashirika hayo kama wadau kuna nafasi kubwa ya kutatua changamoto hizo.
“Lakini pia tunachangamoto ya makundi ya vijana, vijana wengi Dodoma wako mtaani, sisi kama Serikali na nyinyi kama wadau tushirikiane kuhakikisha vijana wale wanaenda kufanya kazi kwa ajili ya uchumi wa Tanzania, Rais ameweka miradi mingi sana, Dodoma sasa hivi kila unachokifanya kinaleta faida, kwahiyo tunawajibu kama Mashirika na Serikali kuhakikisha makundi maalumu yanapata vitu vya kufanya” aliongeza Sharifa.
Akiwawakilisha wamiliki wa makampuni yasio ya kiserikali, Mratibu wa mawasiliano wa kampuni ya Buta vikoba endelevu, Adriano Gama aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuitisha kikao hicho kwani kimetoa matokeo makubwa na kimewapa mwanga wao kama wadau ambao wanafanya kazi na wananchi moja kwa moja tofauti na hapo awali ambapo wengi wao walikua wakifanya kazi bila kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu miongozo inayowahusu.
Mratibu wa mawasiliano wa kampuni ya Buta vikoba endelevu, Adriano Gama aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuandaa kikao na wadau kutoka Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.