Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na kampuni ya Green Waste Pro pamoja na taasisi za Elimu wameadhimisha siku ya usafi Duniani kwa kufanya Usafi katika eneo la Majengo Jijini hapa.
Akizungumza na Mwandishi wetu Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti taka ngumu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dickson Kimaro (pichani juu), amesema kuwa ni haki kwa kila mwananchi au mwanadamu kuishi katika mazingira safi na salama hivyo wameamua kufanya usafi kwa vitendo katika eneo hilo ili kutoa elimu kwa wananchi kutambua umuhimu wa kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka.
Kimaro amesema, kumekua na tabia isiyo nzuri kwa baadhi ya wananchi kuchafua mazingira na kukwepa kuyafanyia usafi jambo linalopelekea baadhi ya maeneo ya Jijini hapa kuwa machafu.
Alisema zipo sheria ndogo za Halmashauri ambazo zinamtaka mwananchi kutochafua mazingira kwa aina yoyote ile na kwa atakaekiuka sheria hizo na kukamatwa faini yake ni kuanzia shilingi elfu hamsini mpaka laki moja.
Nae Meneja wa kampuni ya Green Waste Pro Abdala Mbena amesema amefurahishwa na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kufanya usafi kwani kitendo hicho kinaonesha ni jinsi gani wananchi wamepata elimu ya kutosha juu ya usafi wa mazingira.
Mbena ameongeza kuwa wameamua kushirikisha Taasisi za Elimu ili kuwajengea mazoea wanafunzi ya kupenda kufanya usafi kuanzia wakiwa na umri mdogo jambo ambalo linatengeneza kizazi kitakachoweza kuleta matokeo makubwa zaidi kwenye sekta hiyo hapo baadae.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule ya Viwandani Witnes Peter amesema kuwa miongoni mwa athali kubwa zinazotokana na kuzungukwa na mazingira machafu ni pamoja na kupata magonjwa kama vile Kipindupindu na Malaria kwaiyo wamejitolea kuja kuungana na wadau wengine kufanya usafi ili kuilinda jamii isipatwe na magonjwa ya aina hiyo.
Witnes alimalizia kwa kuomba kila Shule iwe na klabu za mazingira kwani kwa kufanya hivyo sio tu mazingira yatakua safi, bali na jamii itapata elimu zaidi ya mazingira kupitia kwa wanafunzi.
Meneja wa Kampuni ya Green Waste Pro Abdallah Mbena akizungumza mara baada ya shughuli za usafi kukamilika.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Viwandani wakishiriki kufanya usafi Siku ya Mazingira Duniani.
Mwanafunzi Witness Peter akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu usafi wa mazingira.
Wananchi wakishiriki kufanya usafi kwenye eneo la 'Pombe River' kata ya Majengo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.