Wakati Watanzania wengi wakiwa na changamoto ya kupata namba ya utambulisho wa Taifa (NIN), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewarahisishia kwa kuweka utaratibu wa kuipata kwa njia ya mtandao.
Taarifa iliyotolewa na NIDA jana Jumatano Septemba 25, 2019 kupitia kitengo cha mawasiliano na hifadhi hati ilisema namba hiyo sasa imeanza kutolewa kupitia tovuti ya mamlaka hiyo kwa muombaji kutembelea https://services.nida.go.tz/nidpotal/get_nin.aspx.
Taarifa ya Nida ilibainisha kwamba huduma hiyo itawarahisishia waombaji wa vitambulisho vya Taifa kupata NIN bila kwenda ofisi za mamlaka hiyo.
Hatua za kufuta kupata namba ya NIN
Aidha Nida imefafanua kuwa namba za NIN pia zimepelekwa ofisi za kata ili kuwapunguzia waombaji adha ya kufuata namba hizo ofisi za Nida za wilaya.
"Waombaji pia wanaweza kupata NIN kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenye kituo cha huduma kwa mteja," ilieleza taarifa hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.