MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Binilith Mahenge ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kulitaka Jiji hilo kujipanga katika usimamizi wake.
Kauli hiyo ameitoa leo alipofanya ziara ya kawaida ya kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Dkt Mahenge alisema “nimejiridhisha na utekelezaji wa miradi yote mitatu inaenda vizuri sana. Mkandarasi Mohammedi Builders unafanya kazi nzuri. Pongezi kwa Mkurugenzi wa Jiji na Mkuu wa wilaya kwa kazi nzuri ya usimamizi”.
Dkt. Mahenge alisema kuwa mafanikio ya miradi hiyo yanatokana na uthubutu wa Rais, Dkt John Magufuli kuhamishia rasmi makao makuu Dodoma na kutenga fedha za kutekeleza miradi hiyo.
Mkuu wa Mkoa aliiagiza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuandaa orodha na michoro ya maeneo ya wazi yote yaliyotengwa katika Mpango kabambe wa mwaka 1976 na kuiwasilisha ofisini kwake. Alisema, Halmashauri ya Jiji inatakuwa kuwa na maeneo ya mapumziko mengi ili kuwapa nafasi wakazi wa jiji hilo kupumzika.
Katika maelezo ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alisema kuwa Halmashauri yake inatekeleza miradi kwa zaidi ya shilingi bilioni 77.8. Serikali imeleta fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati. “Leo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa anakagua soko kubwa la Dodoma, kituo cha mabasi ambacho ni kikubwa Afrika mashariki na mradi wa uboreshaji mandhari ya eneo la kupumzikia ambao haujawahi kutokea Afrika” alisema Kunambi. Miradi yote inayotekelezwa ina hadhi ya makao makuu ya nchi. Miradi yote unayotekelezwa inaenda kwa kasi ya kuridhisha
“Miradi yote hii ina faida kubwa kwa wananchi wa Dodoma na nje ya Dodoma. Mheshimiwa Rais anafanya kazi kubwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Shukrani kwako Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwa kutusimamia vizuri. Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri kwa kazi nzuri. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, usichoke kututembelea na kutupa maelekezo” alisema Kunambi. Halmashauri ya Jiji la Dodoma, tunamuunga mkono Rais, mambo yanaonekana yenyewe, aliongeza Mkurugenzi.
Aidha Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi alisema "Jiji la Dodoma linaenda kuwa kubwa na lakuvutia kwani linajengwa katika karne ya 21 na nitajitahidi kusimamia vizuri ili kupata faida katika miradi yote"
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alikagua miradi ya kimkakati ya uboreshaji wa mandhari ya eneo la kupumzikia (Recreational park) katika eneo la Chinangali, ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi na soko kuu katika eneo la Nzuguni. Katika ziara hiyo aliambatana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Mkuu wa Wilaya Patrobas Katambi na Mratibu wa miradi ya uboreshaji wa Miji ya kimkakati Mhandisi Emmanuel Manyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele),Mkuu wa Wilaya Patrobas Katambi (wa kwanza kulia mstari wa mbele) na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma (wa tatu kutoka kushoto) wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi kutoka kwa Mhandisi kutoka kampuni ya ujenzi ya Mohamed Builders Ltd.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine walipotembelea miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Soko kuu, Kituo kikuu cha mabasi na eneo la kupumzikia, miradi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.