RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema asingekuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa kuchanjwa chanjo ya UVIKO kama ingekuwa si salama.
Rais Samia ameyasema hayo katika uzinduzi wa uchanjaji wa chanjo, hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, ikiwa ni baada ya wiki iliyopita taifa kupokea zaidi ya dozi milioni 1,058,400 za chanjo zilizotolewa kupitia mpango wa upatikanaji wa chanjo Covax.
Rais amebainisha kwa kusema kuwa, “Nimekubali kwa hiyari yangu kuchanja nikijua kwamba ndani ya mwili wangu nina chanjo kadhaa ambazo nimeishi nazo kwa miaka 61 sasa, tangu tumezaliwa tumepata chanjo zisizopungua tano na hii ya sita na nyingine nilizochanja nikiwa safarini, hivyo sioni hatari ya chanjo hii baada ya wanasayansi kujiridhisha na zimekuja nchini na wanasayansi wetu nchini wamejiridhisha mimi niko tayari kuchanja”.
Katika mpango huo, Mhe. Rais amewaondoa hofu wananchi kuhusiana na chanjo, huku akisema yeye ni kiongozi mkuu wa nchi asingejitoa mwenyewe akajipeleka kwenye hatari huku ajikua kuwa ana majukumu yanayomtegemea.
"Mimi ni mama wa watoto 4 wanaonitegemea ni Bibi wa wajukuu kadhaa wanaonipenda sana na mimi nawapenda, ni mke pia lakini mbali ya yote ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya nchi hii nisingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye kifo" amesema Rais Samia.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.