JAMII imeshauriwa kuwahamasisha wanafunzi wa kike kuchangamkia masomo ya sayansi hasa fani za uhandisi wa Ndege ili watoe mchango katika Taifa lao.
Kauli hiyo ilitolewa na Mhandisi Matengenezo ya Ndege kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi Castory Njako alipokuwa akiongea na walimu na wanafunzi waliotembelea banda wa chuo hicho katika maonesho ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Asilimia kubwa ya wanafunzi wanaokuja kujifunza katika fani za uhandisi wa Ndege ni wanaume. “Tunahitaji sana watoto wa kike kuhamasishwa ili wawe na ndoto za uhandisi wa matengenezo ya Ndege. Hamasa hii ifanyike kwa kuwajengea desturi ya wanafunzi kutembelea vyuo na maonesho kama haya kunawajengea hamasa ya kupenda masomo ya sayansi” alisema Mhandisi Njako.
Akizungumzia dhana ya ugumu wa masomo ya sayansi, alisema kuwa dhana hiyo inajengwa kuleta hofu. “Siyo masomo hayo ni magumu, ugumu ni uelewa wanafunzi wanaojengewa na jamii. Kimsingi kila somo ni gumu, hakuna masomo ambayo ni mepesi. Fani ya uhandisi wa Ndege msingi wake ni hesabu, fizikia, kemia na kiingereza” aliongeza Mhandisi huyo.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Ngusekela Daudi alisema kuwa chuo hicho kinatoa ulimu katika fani mbalimbali. Alizitaja fani hizo kuwa ni uhandisi wa Ndege, mitambo, mabomba ya mafuta na matengenezo ya Meli. Nyingine ni usimamizi wa usafirishaji, ualimu ubobezi teknolojia na hesabu, ukutubi na mawasiliano. Aidha, alitoa wito kwa elimu bora watembelee chuo hicho.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendesha Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) kila mwaka kwa madhumuni ya kutambua, kuadhimisha, kujenga, kukuza na kuendeleza ubunifu wa watanzania katika nyanja za sayansi na teknolojia ili kuchangia juhudi za kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanja.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.