Na. Asteria Frank, DODOMA
Timu ya mpira wa miguu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Dodoma Jiji yainyuka goli 6-0 timu ya mpira wa miguu ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 ya Tabora United ndani uwanja wa Jamhuri Jiji la Dodoma katika mechi ya kwanza mzunguko wa pili wa ligi ya NBC Youth League 2024/2025.
Kocha wa timu ya vijana umri wa miaka 20 ya Dodoma Jiji FC, Chido Jeremia alisema hawakuwa na mchezo mzuri kipindi cha kwanza na kipindi cha pili walikuwa na nyakati nzuri kwa jinsi vijana walivyowaelekeza kwa hali ya kuona mapungufu ya wenzao na kuweza kupata magoli hayo.
Alisema kuwa timu inaendelea kuimarika na malengo waliyowawekea yanazidi kupungua maana kadri siku wanavyocheza mechi wanapata alama. “Vijana wametuheshimisha tumepata ushindi na sio tu matokeo mazuri ila matokeo yenye magoli mengi kama vile tulivyokuwa tunataka maana tulikuwa tunataka kutengeneza ‘margin’ nzuri zaidi ya wanaotufata lakini pia kutengeneza ‘goal difference’ ambayo ndio vijana wametu-offer. Na tunawashukuru mashabiki hawakuwa nyuma kwa kuja kuwasapoti vijana wao na wanaona wanavyocheza. Vijana hawa sio wa kwetu peke yetu na jukumu la kuwalea lisibaki kwa halmashauri peke yake au makocha wao ila libaki kwa kila mwana Dodoma aone wivu kuwa ni sehemu ya chagizo kuwa vijana hawa niliwaleo na huku ndipo tunapata wachezaji wazuri watakao kuja kutusaidia Dodoma” alisema Chido
Nae Nahodha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Dodoma Jiji FC, Bakari Mondwe alisema kuwa wanamshukuru Mungu wamemaliza mchezo wao salama na malengo yao katika mzunguko huu wa pili ni kuzidi kufanya vizuri ili waweze kuvuka hatua hiyo. “Tunawaomba mashabiki wazidi kuja kwa wingi na kusapoti timu yao ili tuzidi kufanya vizuri na tunawaahidi hatutawaangusha na kuwapa kitu muhimu ambacho wanakuja kukiona kila siku wanapokuja na tutazidi kufanya vizuri” alisema Mondwe.
Mzunguko wa pili ulianza tarehe 15 Januari, 2025 ambapo Dodoma Jiji FC wanaongoza ligi, msimamo wa kundi ‘A’ katika mzunguko wa kwanza wakifuatiwa na Azam FC kwa nafasi ya pili na Kagera Sugar nafasi ya tatu na nafasi ya nne kushikiliwa na Yanga.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.