Na. Faraja Mbise, DODOMA MAKULU
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma yamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kujenga Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma ambayo italeta tija ya kuwahudumia wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kwa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Afisa Tawala katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Merina Ijiko alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo umekamilika na upo katika hatua ya kipindi cha uangalizi cha mwaka mmoja ambacho kilianza tarehe 10 Juni, 2024 na kuisha tarehe 9 Juni, 2025.
Akiongelea fedha za mradi huo, alisema kuwa jumla ya shilingi 1,242,969,735.30 zimelipwa kwa mkandarasi ikiwa ni asilimia 61.89 ya gharama za mradi hadi sasa. Mkandarasi anadai jumla ya shilingi 578,288,969.19 na mhandisi mshauri ameshalipwa jumla ya shilingi 68,380,000.00 ikiwa ni malipo ya marejeo ya usanifu na usimamizi na anadai jumla ya shilingi 36,365,000. “Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inamshukuru Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Hassan Suluhu kwa kutoa fedha za kujenga Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma yenye hadhi. Hii itaongeza tija ya kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Dodoma” alisema Ijiko.
Utekelezaji wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ulianza mwaka wa fedha 2022/2023. Mradi ulijumuisha ujenzi wa jengo kuu la ghorofa moja, kibanda cha mlinzi, uzio wa ukuta wa tofali, mifumo ya CCTV, ‘plumbing works’, mifumo ya uzimaji moto, viyoyozi, ‘electrical works’ na ‘landscaping’ utekelezaji huo unatekelezwa na Mkandarasi Azhar Construction Co. LTD na kusimamiwa na Mhandisi Mshauri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia BICO.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.