Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, ametangaza kuwapangia vituo vya kazi walimu wapya wa sekondari na mafundi sanifu wa maabara 2,160.
Akitangaza vituo vya kazi vya walimu hao jana Jijini Dodoma, Waziri Jafo amesema walimu hao ni sehemu ya ajira za walimu 6,785 ambao Ofisi ya Rais - TAMISEMI ilipata kibali cha kuwaajiri kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora mwezi Mei mwaka huu, ambapo walimu 4,840 walipangiwa vituo vya kazi mapema mwezi Julai mwaka huu.
“Leo tunawatangazia ajira za watumishi 2,160 waliopangwa katika shule za Sekondari 1,721 ambapo kati yao, walimu 1,900 ni wa masomo ya Sayansi na Hisabati, walimu 100 ni wa Kiingereza na Fundi Sanifu Maabara ni 160”
Amesema watumishi hawa waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri husika na baadaye kwenye shule kuanzia tarehe 23 Agosti, 2018 hadi Septemba 5, 2018, huku wakiwa na vyeti halisi vya kitaaluma, na cheti cha kuzaliwa.
Waziri Jafo amewaelekeza Wakurugezi wa Halmashauri ambazo zimepangiwa watumishi hao kuwapokea kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa Umma katika kukamilisha taratibu nyingine za ajira ya watumishi hao wapya.
Amewataka watumishi hao wapya kutochukua posho ya kujikimu bila kuripoti katika kituo cha kazi kwani watachukuliwa hatua za kisheria, wala hakutakuwa na kubadilisha kituo cha kazi kwa sababu yoyote ile, badala yake muda uliotolewa kuripoti ukipita, nafasi hiyo itachukuliwa na mtu mwingine mwenye sifa stahiki ambaye hakuchaguliwa.
Kuona majina ya watumishi walimu wa shule za sekondari waliopangiwa vituo vya kazi Bofya kiunganishi hapa chini:
Chanzo: Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI www.tamisemi.go.tz
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.