Na. OR-TAMISEMI, Dodoma
NAIBU WAZIRI wa Afya Dkt. Godwin Moleli amezitaka Mamlaka za Serikali ngazi ya Wizara, Mikoa, Halmashauri na Taasisi zinazohusika na Sekta ya Afya kutokuwa kikwazo ili kuchochea uwekezaji kwenye Sekta ya Afya nchini.
Dkt. Moleli ametoa kauli hiyo wakati akifunga mkutano wa kimataifa wa Afya ya Msingi uliofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 27 hadi 27 Machi, 2024 Jijini Dodoma ambao umewaleta pamoja Wadau wa ndani na nje ili kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu mafanikio, changamoto na uwekezaji katika afyamsingi kwa lengo la kuboresha huduma za afya kuelekea afya kwa wote Tanzania.
“Sekta Binafsi imesaidia kwa kiwango kikubwa kuipunguzia Serikali mzigo hasa upande wa ajira kwani vijana wengi wameajiriwa kupitia sekta binafsi, hali ambayo sio rahisi kuiachia mzigo Serikali pekee, taste tuliyonayo sio ajira siyo Serikali peke yake” alisema Dkt. Mollel
Dkt. Moleli pia amezitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Afya kufuatilia na kujua ni vijiji vingapi nchini ambavyo havina zahanati ili kuendelea kuboresha afyamsingi nchini lakini pia amewataka wataalam wa wizara hizo mbili kuangalia sheria zinazohusu uanzishwaji wa zahanati ili kuondoa vikwazo kwa wawekezaji kama idadi ya waajiriwa ili kituo kitoe huduma.
Naye Dkt. Wilson Mahera Charles, Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI alisema baadhi ya mapendekezo makubwa yaliyotokana na mkutano huo ni kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa afyamsingi, kuongeza bajeti za afya na kukuza mifumo ya Bima za Afya.
Akitoa salamu za Wadau, Agnes Cosia kwa niaba ya Sekta ya Afya binafsi (Christian Social Services Commission) alisema vituo binafsi vimechangia kupunguza vifo vya mama na mtoto, kupunguza kasi ya maambukizo ya vifo vinavyotokana na magonjwa ya mlipuko na kuchangia juhudi za pamoja za Serikali na Wadau wengine kuhakikisha upatikanaji wa afya bora kwa watu.
Dkt. Rashid Mfaume Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI alisema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2023 asilimia 78 ya wagonjwa wa nje (OPD) wametoka eneo la afya ya msingi
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.