Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Mfuko wa Misaada kutoka nchi zinazozlisha na kusambaza mafuta duniani (OPEC), Shoragim Shams, ameupongeza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa kusimamia vyema fedha za miradi zinazotolewa na mfuko huo.
Shams alitoa kauli hiyo jana mjini Arusha katika ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Shule ya Sekondari Oldonyowas katika Kijiji Cha Oldonyowas mkoani Arusha.
Alisema utoaji fedha za miradi ni jambo moja, lakini utekelezaji ni jambo jingine ambalo TASAF wamefanikisha kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.
"Sisi tumetoa fedha kwa lengo la kusaidia jamii, lakini zisingeweza kusaidia chochote endapo kusingekuwapo usimamizi thabiti na wananchi wenyewe kujitolea nguvu zao.
"Nimetembelea na kushuhudia kilichofanyika ni kizuri na OPEC tunaipongeza TASAF na kuahidi kuendeleza kushirikiana nanyi katika awamu nyingine inayofuata," aliahidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Taifa, Ladislaus Mwamanga, alisema mwakilishi huyo wa OPEC amekuja kuangalia utekelezaji wa miradi hiyo awamu inayomalizika kwa lengo la maaandalizi ya awamu nyingine inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Alisema katika awamu inayomalizika, mambo mengi yamefanyika kwa ufadhili wa wadau hao katika maeneo ya uboreshaji miundombinu ya elimu, afya, maji na barabara.
"Katika Shule hii ya Sekondari Oldonyowas zaidi ya Sh. milioni 470 zimetumika katika ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, mabweni na matundu ya vyoo," alisema.
Mwamanga aliwapongeza wananchi kwa kujitoa katika nguvu kazi na kusisitiza utekelezaji wa miradi unahitaji ushirikiano na wananchi ili kuzalisha ajira za muda zitakazojitokeza alisisitiza Mkurugenzi huyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.