Zoezi la kuondosha vibanda vilivyojengwa juu ya mtaro wa maji ya mvua na usafi katika Soko la Sabasaba uliofanyika leo Jumamosi umefanikiwa kwa sehemu kubwa. Wafanyabiashara waliokuwa wamejenga juu ya mtaro wa mji ya mvua na kusababisha mitaro hiyo kuziba na kuwa kero kwa watumiaji wa soko na wafanyabiashara, waliviondoa wenyewe vibanda hivyo na kuruhusu usafi kufanyika.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro alipokuwa akitoa taarifa fupi juu ya utekelezaji wa zoezi la kuweka mazingira ya Soko la Sabasaba na maeneo mengine ya Jiji la Dodoma kuwa safi hususani kipindi hiki ambacho suala la usafi ni la muhimu sana ili kudhibiti maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwamo ugonjwa wa Covid-19 unaosababishw na virusi vya Corona.
Wafanyabiashara wa soko la Sabasaba wakishiriki kuondosha vibanda vilivyokuwa vimejengwa kuu ya mtaro wa maji ya mvua.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.