• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

OR-TAMISEMI wafafanua utaratibu wa kuwapata wanafunzi wa bweni

Imewekwa tarehe: January 4th, 2023

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI anayesimamia Elimu, Dkt. Charles Msonde  amesema kuna vigezo wazi ambavyo vinatumika kuchagua wanafunzi hao.

Dkt. Msonde ametoa ufafanuzi huo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ya  kukagua ujenzi wa miundombinu ya madarasa yatakayopokea wanafunzi wa kidato cha kwanza,2023.

Alisema kuwa wanafunzi waliofaulu na kuwa na sifa ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  mwaka 2023 ni 1,073,941 na kati ya hao waliochaguliwa kujiunga na shule za bweni ni 4,224  ambao ni sawa na asilimia 0.39 ya wanafunzi wote waliochaguliwa.

Akifafanua ni kwa nini idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kwa shule za bweni ni ndogo, Dkt. Msonde alisema ni kutokana na ufinyu wa shule za bweni,

Alisema kuwa idadi ya shule za Sekondari za Serikali zinazochukua wanafunzi wa kidato cha kwanza ni 4,307 na kati ya hizo shule za kutwa ni 4,269 na za bweni ni 38 tu ambazo zinauwezo wa kuchukua wanafunzi 4,224.

"Kutokana na idadi ndogo ya shule za bweni tulizonazo na ili watoto waweze kukaa darasani vizuri, kulala bwenini kwa mujibu wa muongozo, shule hizo 38 zina uwezo wa kupokea wanafunzi 4,224 ambao ni sawa na asilinia 0.39 tu ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza."

Akizungumzia namna ya kuwapata wanafunzi kujiunga na shule za bweni, uchaguzi wa wanafunzi hao umekuwa ukizingatia vigezo mbalimbali ikiwemo ya kuzingatia viwango vya ufaulu.

"Wale wenye viwango vya juu sana ndio waliochaguliwa, lakini hata hivyo waliofaulu kwa viwango vya juu pia ni wengi, hivyo mfumo ulitumika kuchagua wale waliofauli zaidi ya wenzao."

“Hapa tunasema waliochaguliwa kwenda bweni wamepata daraja la kwanza A, lakini ukiangalia waliopata daraja hilo wapo wanafunzi 50,475, hivyo hata kwenye daraja hili la kwanza ipo kanuni iliyotumika ya kugawa nafasi za wanafunzi waliofaulu vizuri."

Alisema  kuwa, shule za bweni zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni  kundi la kwanza ni lile lenye ufaulu wa juu, kundi la pili ni shule za bweni za ufundi na kundi la tatu ni shule za bweni kawaida.

Dkt. Msonde alisema kwa upande wa shule zenye ufaulu wa juu ziko saba zikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 932 ambao ndio waliopangiwa.

Pia, shule za bweni za ufundi ziko tisa zikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,323 wakai shule za bweni za kawaida zimechukua wanafunzi 1,816 na bweni umiliki wa mkoa 153.

" Ikumbukwe kuwa shule hizi za bweni ni za Kitaifa, hivyo uchaguzi wa wanafunzi wa kwenda katika shule hizo pia unafanyika kitaifa kwa maana kuwa kila mkoa na halmashauri nchini lazima zitoe wanafunzi watakaokwenda kusoma katika shule hizo."

"Hapa tunaona wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja kwanza (A) wako 50,475 na kati ya hao waliochaguliwa ni 4,224, hivyo kwenye shule za bweni zenye ufaulu wa juu tunatumia uwiano wa idadi wa watahiniwa katika mkoa  mara Idadi ya nafasi zote kwa watahiniwa waliofaulu zaidi gawanya kwa jumla ya watahiniwa wote kitaifa hapo utapata  idadi ya nafasi za bweni kwa watahiniwa waliofaulu zaidi kwenye Mkoa."

Dkt. Msonde aliongeza, "kanuni hiyo hiyo itatumika kwenye mkoa kupata idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kwenda kwenye shule zenye ufaulu wa juu kutoka mkoa husika."

"Kanuni hii pia itatumika kupata wanafunzi waliochaguliwa kwenye shule za bweni za ufundi kutoka kwenye mikoa yote nchini."

Kwa upande wa shule za bweni kawaida, Dkt. Msonde alisema kanuni yake ni uwiano wa watahiniwa wote wa Darasa la Saba katika shule za vijijini au mazingira magumu katika Halmashauri mara idadi ya nafasi zote za bweni kwa wavulana na wasichana wa vijijini au mazingira magumu Tanzania bara gawanya na idadi ya watahiniwa wote wa darasa la VII katika shule za vijijini/mazingira magumu hapo utapata nafasi kwa kila Halmashauri.

"Ikumbukwe kuwa nafasi hizi ni kwa wanafunzi wote waliosoma shule za Serikali na Binafsi katika Mkoa na Halmashauri husika."

Dkt Msonde alisema kwa shule za kutwa wanafunzi  1,069,717  walichaguliwa kwenda kwenye shule hizo ambapo kila wanafunzi aliyefaulu na kukosa nafasi kwenye ushindani wa shule za Bweni alipangiwa kwenye shule ya sekondari ya kutwa  iliyokaribu na shule ya msingi aliyosomea.

"Sambamba na kanuni na muongozo wa uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mfumo ndio uliotumika kufanya chaguzi hizo hii kupunguza changamoto za kibanaadamu ambazo zingeweza kuleta mgongano wa kimaslahi."

Dkt. Msonde aliongeza kuwa: "kila mwanafunzi aliyechaguliwa kwenda shule ya bweni anakidhi vigezo vyote hata ukiingia kwenye mfumo utaona kuwa vigezo vyake ni vya juu kuliko wengine waliokwenda kwenye shule za kutwa katika hili  watoto wa Taifa hili kutoka pembe zote za nchi wenye vigezo wamechaguliwa kwenda kwenye shule za bweni ili kuleta utaifa na umoja kwa watoto wetu.

Alisema daraja la  A analipoata mwanafunzi ni kati ya jumla ya alama 241 hadi 300.

"Niweke wazi kuwa ufaulu wa daraja la kwanza yaani A unaanzia kwenye maksi 241 hadi 300,, na wazazi au walezi wanaona daraja ambalo mtoto wake amepata lakini sisi tunaoingia kwenye mfumo tunaona alama  sasa mtaona kwamba takribani wanafunzi  46,251 wenye ufaulu wa daraja la kwanza (A) wamepangiwa kwenye shule za kutwa kutokana na uhaba wa nafasi za bweni.

"Lakini wale waliopangiwa bweni wanaufaulu wa daraja la kwanza wa alama za juu zaidi kuliko wale 46,251 na ndio maana tulivyofika ukomo wa idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kwenda bweni wale waliobakia wenye ufaulu wa daraja la kwanza wote waliopangiwa kwenye shule za kutwa."

Aidha, Dkt. Msonde alitumia fursa hiyo kuwasihi wazazi kuhakikisha wanafunzi wote waliopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza, 2023 wanaripoti shule kwa wakati ili waweze kuanza masomo kwa awamu moja.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.