Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma anawatangazia Wananchi wote kuwa, Halmashauri imekamilisha upimaji wa viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo makazi, biashara, makazi na biashara, taasisi mbalimbali, sehemu za ibada na viwanda na inaviuza kuanzia tarehe 10 Desemba, 2018.
Viwanja vipo katika maeneo ya Mapinduzi "A", Mtumba, Nala na Medeli Extension ambavyo vina ukubwa wa mita za ujazo tofauti kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Aidha, kwa wale waliochukua viwanja awali katika eneo la Mtumba, Kikombo na Iyumbu lakini hawajavilipia, viwanja hivyo vinauzwa upya kuanzia tarehe tajwa hapo juu bila wahusika kupewa taarifa yoyote.
Zoezi la uuzaji viwanja linafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi katika eneo la wazi kwenye Ofisi za Jiji zilizopo jirani na Sabasaba (Ofisi Kuuya Manispaa ya zamani).
Kila anayehitaji kiwanja afike Ofisi za Jiji kwa ajili ya kufanya taratibu kuanzia tarehe tajwa,na anatakiwa kukamilisha malipo yote ndani ya miezi mitatu (yaani siku 90) kuanzia tarehe atakayopewa ankara ya madai.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.