• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

PM awaagiza Ma-RC, Ma-DC watatue migogoro ya ardhi

Imewekwa tarehe: February 10th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Watendaji wa Kata waweke utaratibu wa kusikiliza na kutatua kero za migogoro ya ardhi katika maeneno yao badala ya kusubiri viongozi wa kitaifa au Mawaziri.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Februari 10, 2022 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini, Mheshimiwa Oran Njeza aliyetaka kujua ni lini Kamati ya Mawaziri itarejea kukamilisha migogoro kati ya wananchi na TANAPA na TFS kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

“Nitoe wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Watendaji wa Kata na viongozi wote kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa wafike maeneo hayo. Natambua kuna migogoro ya mipaka kati ya vijiji na vijiji, pia ipo ya wafugaji na wakulima, hakikini migogoro hii na muikamilishe huko huko badala ya kusubiri Mawaziri wasafiri kuja huko, kila mmoja akiwajibika migogoro hii itapungua kwa kiasi kikubwa” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu ameiagiza kamati ya Mawaziri nane iliyoundwa kwa ajili ya kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi kuweka mpango kazi wa kwenyda Mbeya Vijijini wakaangalie aina ya migogoro iliyopo na nini kifanyike baada ya kuhakiki.

Akijibu swali ya Mheshimwa Leah Komanya aliyetaka kujua mkakati wa Serikali katika kukabiliana na ukame hasa kwenye eneo la malisho ya mifugo, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi ikiwemo misitu ili isaidie kuleta mvua na kukabilana na ukame.

“Kutokana na ukame hatuwezi kupata malisho, hivyo ni lazima tuhifadhi mazingira ili malisho yapatikane, pia wizara ya mifugo inatoa elimu kwa wafugaji ikiwemo uwaeleza kwa wafuge kitaalam kulingana na ukubwa wa malisho waliyo nayo ili kukabiliana na upungufu wa malisho unaotokana na uwepo wa mifugo mingi”.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania waache tabia ya kukata miti katika maeneno yao ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na ukame ili misitu hiyo iweze kusaidia kupatikana kwa mvua za kutosha. “Ndugu zangu wafugaji endeleeni kufuga kitaalam, kuweni na mifugo michache mnayoweza kuihudumia badala ya kuwa na mifugo mingi msiyoweza kuimudu.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaoweka mkakati wa kusumbua jamii kwa kuuza bidhaa kwa bei ya juu. “Serikali tunaweka mazingira rafiki ya uwekezaji lengo ni kusaidia upatikanaji wa bidhaa kwa wingi, bei nafuu na wakati wote, na tutaendelea kulifanyia kazi hili kupitia taasisi zetu za Serikali”.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kudumisha amani na usalama ili kuwawezesha wenye nia ya kufanya biashara wakati wowote ikiwemo nyakati za usiku kufanya hivyo. “Malengo yetu ni kuboresha uchumi wan chi, kama nchi haipo salama hatuwezi kufikia malengo.”

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.