WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa leo Novemba 30, 2020 amepokea taarifa ya utuatiliaji wa mwenendo wa vyama vya ushirika vya NCU (1984) Ltd, KNCU (1984) Ltd na SHIRECU (1984) Ltd kutoka kwa timu maalum ya uchunguzi aliyoiunda.
Katika hafla hiyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa vyama vya ushirika nchini wabadilike na wawe na weledi ili kurejesha heshima ya ushirika nchini. "Viongozi wa ushirika ni lazima tubadilike. Nyie mliopewa dhamana kwenye vyama vikuu hivi vitatu vya KNCU, NYANZA na SHIRECU lazima mbadilike, nyie mmepewa dhamana ya kuwasaidia Watanzania wenzetu wanyonge wanaolima ekari moja, mbili au tatu". Amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.
Mapema akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, kiongozi wa timu hiyo maalum, bwana Asangye Bangu alisema timu hiyo imefanikiwa kurejesha mali 60 za ushirika zenye thamani ya 68.98. Mali hizo zinajumuisha majengo, viwanja, magari na mitambo ya machine, hazikuwa mikononi mwa vyama hivi vitatu lakini sasa zimerudishwa kwenye umma.
Picha na matukio:
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.