WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo Agosti 28, 2021 ameanza ziara katika Mkoa wa Tabora kwa kutembelea Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora "Tabora School" na Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora "Tabora Girls".
Aidha, katika ziara hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amekagua ujenzi wa majengo yaliyokarabatiwa ikiwemo mabweni na maktaba na kisha kupata nafasi ya kuongea na wanafunzi na walimu ambapo ameelezea kuhusu mikakati mbalimbali ya Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Ikumbukwe kuwa 'Tabora School' ndiyo shule ambayo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipatia elimu yake ya sekondari kati ya mwaka 1937 - 1942.
Shule hiyo inahistoria ya kuwa na viongozi na watu wengi maarufu waliosoma hapo na miongoni mwao ni Rashid Mfaume Kawawa, Kaluta Amri Abeid, Oscar Kambona, Prof. Ibrahim Lipumba, Dkt. Harrison Mwakyembe, Juma Mwapachu, Dkt. David Mwakyusa, Makongoro Nyerere, Jaji Mstaafu Barnabas Samatta, Spika Mstaafu Samuel Sitta, Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Brigedia Gen. Hashim Mbitta, Jaji Mst. Augustino Ramadhani, Edwin Mtei, Tuntemeke Sanga na wengineo wengi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.