Na. Dennis Gondwe, DODOMA
BENKI kuu ya Tanzania imepongezwa kwa jinsi inavyosimamia uchumi wa nchi na kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wadogo nchini.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Khamis Mkanachi baada ya kutembelea banda la Benki Kuu na kupokea maelezo kutoka kwa maafisa waandamizi katika maonesho ya shughuli za wakulima na wafugaji kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Dkt. Mkanachi alisema kuwa msafara wake umefarijika jinsi benki hiyo inavyosimamia uchumi wa nchi. “Katika maelezo yenu mmeelezea jinsi mnavyowashirikisha wafanyabiashara wadogo. Tumefurahi sana jinsi mnavyowajali wafanyabiashara wadogo. Pia nichukue nafasi hii kuwapongeza jinsi mnavyosimamia uchumi wa taifa. Uchumi upo imara kutokana na ninyi kuwa imara” alisema Dkt. Mkanachi.
Maonesho ya shughuli za kilimo na mifugo mwaka 2022 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Agenda 10/30: kilimo ni biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.