KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Prof. Riziki Shemdoe ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze , Mkoani Pwani
Pro.Shemdoe amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo
Amekagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi watakaoanza masomo ya kidato cha kwanza Januari 2023, ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Chahua,na shule ya Sekondari Lugoba.
Prof. Shemdoe ameipongeza Halmashauri hiyo kwa usimamizi wenye weledi wa kuhakikisha madarasa hayo yanajengwa kwa viwango stahiki.
“Nikupongeze Mkurugenzi na timu yako kwa usimamizi makini, madiwani na uongozi wa Shule kwa maana ya wakuu Shule wote wanaoendelea na utekelezaji wa miradi hii nawaomba muongeze bidii mara ifikapo tarehe 15 Desemba, madarasa yawe yamekamilika.” amesisitiza Prof Shemdoe
Vilevile, Prof. Shemdoe amekagua Ujenzi wa soko la Bwilingu na kukagua ujenzi wa vibanda vya wajasiriamali vinavyoendelea kujengwa kuzunguka soko jumla ya vibanda hivyo ni 150 na vinajengwa kutokana fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuwezesha wananchi kiuchumi.
Pia Prof Shemdoe amekagua hospitali ya Wilaya ya Msoga na kukagua Ujenzi wa jengo la Matibabu ya Dharura(EMD) kinachoendelea kujengwa katika hospitali hiyo na kumshukuru Rais Mstaafu wa awamu Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwezesha upatikanaji wa mradi huo unaotekelezwa kwa faida ya watanzania wanapopatwa na ajali na kuwa na uhakika wa matibabu wakati wowote.
Aidha, amekagua vifaa tiba mbalimbal vilivyonunuliwa kutokana na fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri na fedha kutoka Serikali kuu ambavyo ni vifaa vya Mionzi (X-ray)na vipimo vya moyo vinavyopima umeme wa moyo kwa binadamu.
Amewapongeza viongozi wa Halmashauri kwa hatua kubwa za maendeleo zinazofanywa hasa katika suala zima la usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.