KAMATI ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewataka wafanyabiashara waliovamia eneo la shule ya sekondari Viwandani jijini hapa kuondoka eneo hilo ili kuwawezesha wanafunzi kusoma vizuri.
Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe kwa niaba ya ya wajumbe alipoongoza kamati ya fedha na utawala kutembelea shule hiyo jana mchana.
Prof. Mwamfupe alisema kuwa shule ni eneo kwa ajili ya wanafunzi kujifunza si eneo la wafanyabiashara. “Hatutaki kuona biashara yoyote eneo la shule. Tunataka watoto wetu wajikite kusoma sio muingiliano wa masomo na biashara jambo linalochangia watoto kuzurura nje na kudhoofisha ufanisi kitaaluma. Tusitumie vibaya dhamira njema ya Mhe Rais kuwatengenezea mazingira rafiki wafanyabiashara kufanya kazi zao. Mhe Rais hajasema wafanyabiashara wafanye biashara katika maeneo ya shule” alisema Prof. Mwamfupe. Shule ziachwe kuwa sehemu salama kwa ajili ya wanafunzi kusoma, aliongeza.
Naye Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Happiness Matonya alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri hiyo ilipeleka shilingi milioni 40 kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha maabara ya shule ya sekondari Viwandani.
Akichangia zaidi mjumbe wa kamati hiyo, Mhe. Paskazia Mayala alipongeza ushirikiano ambao kamati hiyo inaupata kutoka kwa wataalam wa Halmashauri jambo lililofanya ukaguzi huo kuwa rahisi. Aidha, alimpongeza mstahiki Meya kwa kuwaongoza vizuri madiwani jambo ambalo linawezesha Jiji la Dodoma kupiga hatua katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Viwandani wakifanya majaribio ya kisayansi kwenye maabala ya shule iliyojengwa kwa fedha za makusanyo ya ndani ya Jiji la Dodoma.
Mwonekano wa jengo jipya la maabara la shule ya sekondari Viwandani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.