Na. Dennis Gondwe, HOMBOLO MAKULU
WANANCHI wa Kata ya Hombolo Makulu wametakiwa kumshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha watoto wao wanasoma kwa bidii katika shule iliyojengwa na serikali ya awamu ya sita katika kata hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe alipotoa salamu kwa wananchi wa Kata ya Hombolo Makulu jijini Dodoma katika ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Dodoma.
Prof. Mwamfupe alisema “wito wangu kwa wananchi wa eneo hili la Hombolo Makulu hatuna namna yoyote ya kufunga safari kwenda Dodoma au Dar es Salaam kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tumshukuru tukiwa hapahapa kwa kuhakikisha watoto wetu wanatumia miundombinu ya elimu iliyojengwa shuleni hapa. Kumbuka sisi katika misingi ya elimu bado hatupo katika namba nzuri, moja wapo ya sabau zilizochangia ni ukosefu wa miundombinu. Sasa miundombinu imejengwa, shule zipo hapa tulitegemea idadi kubwa ya watoto shuleni hapa itoke hapa katika kata hii”.
Mstahiki Meya aliitaka Kamati ya shule hakikisheni majengo yaliyopewa thamani yanatunzwa vizuri ili yadumu muda mrefu. “Walimu tunategemea watoto waliokuwa wanatembea umbali mrefu kiwango cha ufaulu kinakwenda kuongezeka” alisema Prof. Mwamfupe.
Nae Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga aliwapongeza wananchi wa kata ya hombolo makulu kwa kuendelea kuchapa kazi na kuwaahidi kuwa serikali yao itaendelea kuwapelekea maendeleo.
“Leo tumepokea taarifa kuwa kata hii wamepata shilingi 95,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu ‘two in one’. Vilevile, wamepokea shilingi 216,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita. Mheshimiwa Diwani ametuambia wamepokea mradi wa Shule mpya ya Msingi Mayeto. Hizi zote ni juhudi za Rais wetu kuwapenda wananchi wake na kuwasogezea maendeleo” alisema Mbaga.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Hombolo Makulu, Gideon Nkana alimshukuru Rais kwa miradi ya maendeleo inayopelekwa katika kata yake. “Ninamshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo ametuheshimisha. Kata ya Hombolo Makulu ilikuwa ni miongoni mwa kata ambazo hazikuwa na miundombinu ya elimu ya sekondari. Ametutendea haki ametujengea shule kubwa lakini ametuletea madarasa nane kwa ajili ya kidato cha tano na sita” alisema Nkana.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.