Na. Asteria Frank, DODOMA
WANANCHI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuchukua tahadhari za afya na usalama barabarani katika maeneo yanayo wazunguka kuelekea msimu huu wa Sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya 2025.
Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, wakati akitoa salamu za kuwatakia wananchi wote na watumishi wa halmashauri, kheri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2025 na kuwaasa kuwa makini kipindi hicho cha sikukuu.
Alisema kuwa wazazi wanatakiwa kuwalinda watoto wao msimu huu wa sikukuu na kufanya maandalizi mazuri ili kuhakikisha wanawaandaa watoto kupata elimu bora ambayo ni haki yao ifikapo mwaka mpya wa masomo 2025. “Nichukue nafasi hii kuwatakia wananchi wote na watumishi kheri ya Krismasi na Mwaka mpya, 2025 nina imani kuwa Mungu kawajaalia kufika hatua kama hii. Sambamba na hilo tunajua Dododma ni mahali shwari, ila tusiache kuchukua tahadhari za kiusalama na wala tusiwaache watoto watembee peke yao. Lakini tukumbuke kuwa msimu kama huu unaambatana na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kusherehekea sikukuu na mkumbuke ni msimu wa mvua. Hivyo, mimi naomba niwasihi sana mchukue tahadhari” alisema Prof. Mwamfupe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.