• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Prof. Mwamfupe; Taka ni fursa ya kutengenezea mbolea

Imewekwa tarehe: January 22nd, 2025

Na. Aisha Haji, DODOMA

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira na kutumia takataka zinazotokana na mazao kama fursa ya kutengeneza mbolea ili kuweza kuinua sekta ya kilimo na uchumi wa halmashauri kiujumla.

Aliyasema hayo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakati wa majadiliano na Kamati ya Ushauri ya Wilaya iliyokutana kupitia mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Akizungumza kuhusu umuhimu wa mbolea zitokanazo na takataka za mazao, alisema kuwa taka za mazao ambazo zinaoza kwa urahisi ni fursa nzuri sana ya kiuchumi kuweza kutengeneza mbolea. Pia alidokeza kuwa halmashauri imejipanga katika suala la kutoa mikopo, mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa wananchi kuhusu namna ya kutumia taka zitokanazo na mazao kwa ajili ya kutengeneza chakula cha kuku kwa kufuata utaratibu maalumu.

Prof. Mwamfupe alisema “halmashauri itakuwa tayari kupitia taratibu zake za kutoa mikopo lakini vilevile, kutoa ushauri wa kitaalamu wa namna ya kutumia taka zinazotoka kwenye masoko yetu kwa ajili ya kutengeneza chakula cha kuku”.

Aidha, aliongeza kuwa wajumbe wajitokeze katika kuchangia  maoni na ushauri katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ili kutambua mambo mbalimbali yanayowakumba wananchi na kupendekeza masuluhisho. “Ningetamani sana michango ya watu kama hivi iweze kujitokeza mara kwa mara. Michango hii tunayoipata hapa tunafurahi kwamba tungekuwa tumepata hata kabla ya wakati huu kwenye vikao vingine kwa ajili ya kuongelea maslahi ya wananchi” alisema Prof. Mwamfupe.

Sambamba na hayo alifafanua kuwa kuna umuhimu wa kuzingatia suala la kupanga bajeti katika mambo mbalimbali kwasababu bajeti yeyote inaundwa kwa kujumuisha mapato na matumizi. “.....bajeti inaundwa na hesabu ya makusanyo sawasawa na matumizi yaani kukiwa na senti moja, senti ishirini imezidi upande mmoja hiyo bajeti imeshindwa” alisema Prof. Mwamfupe.

Vilevile, alitoa rai kwa wajumbe na wananchi wote kwa ujumla kushirikiana na kuhamasishana katika suala la kulipa kodi, kukata leseni na kuchangia michango katika vyanzo mbalimbali vya mapato ili kukamilisha vizuri bajeti ya serikali.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.