KATIBU MKUU Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe (pichani juu) amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanazisimamia Halmashauri kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani na usimamizi wa fedha zinazotolewa na Serikali katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Akifungua kikao kazi cha Makatibu Tawala wa Mikoa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2021/22, Prof. Shemdoe amesema Serikali imepeleka fedha nyingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, hivyo ni wajibu wa Makatibu Tawala Mikoa kuhakikisha fedha hizo zinatekeleza miradi iliyopangwa kwa wakati.
Amewaagiza Maktibu hao kuhakikisha makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri yanakusanywa kwa ufanisi na kutekeleza miradi ya maendeleo kama ilivyopangwa.
Aidha, amewasisitiza wahakikishe Halmashauri zinakamilisha majibu ya hoja za ukaguzi zilizotolewa na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Vilevile, amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha Kamati za Fedha za UVIKO -19 ziundwe kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Ameendelea kufafanua kuwa likizo za Mwaka za Wakurugenzi na Makatibu Tawala zitatolewa kuanzia mwezi Januari, 2022 baada ya ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa, hivyo kiongozi atakaekamilisha kabla ya hapo ataruhusiwa kwenda likizo.
“Hata mimi sitaenda likizo mpaka ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa umekamilika hivyo hakikisheni mnakamilisha ujenzi huo kwa wakati.” amesisitiza Prof. Shemdoe.
Chanzo: ortamisemi (instragram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.