MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kuwa mabalozi wa masuala ya lishe kwa wananchi wanaowaongoza ili kukabiliana na changamoto ya lishe.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Balthazar Ngowi alipokuwa akitoa salamu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani wa Halmashauri ya jiji hilo yanayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Ngowi alisema kuwa Halmashauri imeandaa mafunzo hayo kwa madiwani ili kwa nafasi yao wafikishe elimu hiyo kwa wananchi. “Waheshimiwa madiwani, masuala ya lishe mnayafahamu, ila mafunzo haya yanalenga kukumbushana changamoto za lishe katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma” alisema Ngowi.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Semeni Juma alisema kuwa suala la lishe linatakiwa kuwa agenda ya kudumu katika vikao kwenye kata. “Mafunzo haya yatumike kuhamasisha katika Kata zetu. Maeneo mengi yanakabiliwa na tatizo la utapiamlo sugu” alisema Juma.
Akifafanua kuhusu malengo ya mafunzo hayo, aliyataja kuwa ni kuongeza uelewa na stadi za masuala ya lishe pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa afua muhimu za lishe. Malengo mengine, afisa lishe huyo aliyataja kuwa ni kuongeza uelewa wa makundi maalum na kuhakikisha yanapewa kipaumbele katika afua za lishe. Pia, kuboresha hali ya lishe na afya ya jamii.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Semeni Juma akitoa mada kuhusu lishe kwenye semina ya madiwani wa Jiji la Dodoma leo.
Waheshimiwa madiwani wakimsikiza Afisa Lishe wa Jiji Semeni Juma (hayupo pichani) wakati wa semina inayohusu lishe.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Baltazar Ngowi (aliyesimama) akisisitiza jambo katika mafunzo kwa madiwani kuhusiana na lishe. Kulia ni Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Jumanne Ngede na kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Situ Muhunzi
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.