RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Disemba 24,2020 amemwapisha kamishna wa Maadili Jaji Sivangilwa Mwangesi huku akitoa maagizo kwa watumishi wote kuhakikisha wanakamilisha kujaza fomu za maadili ya utumishi wa umma kabla ya tarehe 30,Disemba ,2020.
Akizungumza mara baada ya uapisho huo uliofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa ifikapo Disemba 30,2020 watumishi wote wahakikishe wanakamilisha kujaza fomu kabla ya tarehe 30, 2020.
Aidha, Rais Dkt.Magufuli ametoa maagizo kwa tume ya Maadili kuacha kurudisha fomu kwa njia ya mtandao ili kuepuka wahalifu wa mtandao wanaoweza kughushi na kuleta mtafaruko.
Kamishna wa maadili Sivangilwa Mwangesi ameahidi kutekeleza majukumu yote aliyopewa kwa kufuata miongozo ya nchi.
Akitoa Salam za pongezi,Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba na Sheria Amon Mpanju ameomba mhimili wa Mahakama kuongezewa nguvu kwa kuongeza majaji huku Naibu Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amebainisha kuwa mpaka sasa karibia asilimia 92 ya watumishi wa umma wanajaza fomu za utumishi wa umma na kutaja mali zao.
Ikumbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Sivangilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili kuanzia Tarehe 23 Disemba 2020 ambapo Jaji Mwangesi anachukua nafasi ya Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Harold Nsekela aliyefariki Dunia hivi Karibuni.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.