Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameahirisha sherehe za Mashujaa zilizokuwa zifanyike tarehe 25 Julai, 2020 jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano Ikulu, Rais Magufuli amewataka Watanzania kutumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea Mashujaa wa nchi hii na pia kuendelea kudumisha amani, upendo, uvumilivu na mshikamano.
Chanzo: @ikulu_mawasiliano (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.