WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi leo tarehe 6 Oktoba, 2020 amefanya Mkutano na waandishi wa Habari na kueleza kuhusu ujio wa Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera nchini Tanzania. Prof. Kabudi amesema Rais wa Malawi anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania tarehe 7 Oktoba, 2020 na atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli. Dkt. Lazarus Chakwera atatembelea bandari ya Dar es Salaam ili kujionea shughuli mbalimbali za bandari hiyo na uboreshaji wa miundombinu ya bandari.
Katika ziara hiyo pia Rais Lazarus akiwa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli wataweka jiwe la msingi katika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani Mbezi mwisho Dar es Salaam.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.