Na. Dennis Gondwe, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha matrekta na zana nyingine za kilimo kwa lengo la kusogeza matumizi ya matrekta karibu na wakulima nchini na kuwapunguzia gharama.
Jiwe hilo la msingi liliweka na Rais katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma.
Akitoa maelezo ya awali, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema kuwa kiwanda cha kuunganisha matrekta na zana nyingine za kilimo ni ushirikiano wa kampuni ya Agricom na Mahindra kutoka nchini India. Alisema kuwa makubaliano baina ya wizara yake na Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini, Angelina Ngalula ni kuwa kampuni hizo kufikia mwezi Juni, 2025 kiwanda hicho kianze kutoa huduma.
Aidha, kiwanda cha kuunganisha matrekta kinajengwa katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni Dodoma eneo lenye ukubwa wa mita za mraba takribani mita za mraba 20,000 kikiunganisha matrekta aina na Swaraj na kutarajiwa kuzalisha ajira za kudumu 400 na ajira zisizo za kudumu zaidi ya 2000.
Kwa upande wa mkazi wa Jiji la Dodoma aliyetembelea maonesho ya Nanenane, Jumanne Siame alisema kuwa maonesho hayo yamechukua sura mpya tofauti na miaka iliyopita. “Mwaka huu tunaongelea kiwanda cha kuunganisha matrekta hapahapa Nanenane. Maana yake huduma hiyo imesegezwa kwa wakulima wa kanda ya kati na gharama za kununua matrekta itakuwa chini tofauti ya ilivyokuwa awali” alisema Siame.
Ikumbukwe kuwa uwekezaji wa kiwanda hicho ni matokeo ya ziara ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India na kualika wawekezaji wa India kuwekeza nchini Tanzania pamoja na mambo mengine.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.