RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli amewashauri wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika mbalimbali ambayo serikali ina hisa kuwekeza katika Jiji la Dodoma.
Ushauri huo ameutoa leo mchana katika hotuba yake baada ya kupokea gawio, michango na ziada kutoka taasisi na mashirika ambayo serikali ina hisa, hafla iliyofanyika katika uwanja wa Ikulu ya Chamwino Dodoma.
Dkt. Magufuli alisema “Wenyeviti na watendaji wakuu msirudi (Dar es Salaam) leo, mzunguke muone sifa na heshima ya Dodoma, muone utamu wa Makao Makuu Dodoma. Ukitaka kuijua Dodoma kaa hapa, mimi nimekaa hapa nimeanza kuisahau Dar es Salaam. Aidha, aliwataka kufikiria uwekezaji katika Jiji hilo. “Anzeni kupanga mipango ya kuwekeza katika Jiji la Dodoma, hapa ndio Makao Makuu ya nchi, na Sheria ipo, hata nikiondoka mimi hakuna wa kuyaondoa Makao Makuu hapa” alisisitiza Rais Dkt. Magufuli. Wale wote ambao bado wanandoto kuwa Dodoma si makao makuu wanajidanganya, aliongeza.
Akiongelea vitambulisho vya wajasiriamali, Rais amesema kuwa wajasiriamali 1,497,033 wamesajiliwa. Aidha, “Jumla ya shilingi bilioni 29,940,660,000 zimekusanywa na hivyo kuongeza wigo wa walipa kodi nchini” amesisitiza Rais Dkt. Magufuli.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.