Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 08 Disemba, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Ikulu Mkoani Dodoma na kuelezea kuridhishwa na kiwango na kasi ya ujenzi wa majengo ya ofisi hizo unaofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Ujenzi wa Ofisi hizo ulioanza tarehe 17 Februari, 2020 unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 3 ijayo na unafanywa kwa usanifu na muonekano saw ana Ofisi za Ikulu zilizopo Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa ujenzi wa ofisi hizo, Luteni Kanali George William Nyisa amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati uliopangwa.
Akikagua majenog yanayojengwa, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na uimara wa nguzo na kuta zinazojengwa na amesema ni fahari kubwa kwa Taifa kujenga ofisi yake ya Ikulu kwa kutumia Jeshi badala ya kutumia wanandarasi kutoka nje ya nchi.
Mhe. Rais Magufuli pia amezungumza na Vijana wa JKT wanaoshiriki jenzi huo ambapo amekumbusha ahadi yake kuwa vijana hao 2,424 wataandikishwa katika JWTZ mara watakapomaliza jukumu la ujenzi wa Ofisi za Ikulu.
Pamoja na kuwapongeza vijana hao, Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza vijana wa kiraia wanaoshiriki katika ujeni huo ambao ni mafundi, na amewaahidi kuwa atawaangalila mara baada ya kumaliza kazi hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.