• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Magufuli arudi Dar, akagua Ubungo 'Flyover'

Imewekwa tarehe: June 19th, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea Makao Makuu Dodoma.

Akiwa Ubungo, Rais Magufuli amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma na kuelezea kufurahishwa kwake na kazi nzuri inayoendelea, pia amewasalimu wananchi wakiwemo viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kando ya eneo la mradi huo.

Akizungumza kwa niaba viongozi wa vyama vya siasa na vijana wa Ubungo, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Ubungo Edwin Cyprian Mbena amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya kutekeleza vizuri na kwa vitendo Ilani ya CCM ikiwemo ujenzi wa barabara za juu katika eneo hilo, na ameeleza kuwa mradi huo umeleta heshima na unawanufaisha wananchi wa Ubungo na Jiji zima la Dar es Salaam.

Amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwaamini vijana na kuwapa nafasi za uongozi na amemuahidi kuwa vijana wamekubaliana kutomuangusha kwa kuhakikisha wanachapakazi na kusimamia maslahi mapana ya Taifa bila kubagua.

Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Ubungo kwa kupata mradi huo na ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inatumia zaidi ya shilingi Bilioni 240 kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo na pia inajenga barabara ya njia nane (Kimara – Kibaha) kwa kuwa imedhamiria kuibadilisha Tanzania. Amewataka Watanzania wote kuunga mkono juhudi hizo.

Baada ya kuwasalimu wananchi hao,  Rais Magufuli aliendesha harambee ya kuchangia ununuzi wa pikipiki ya miguu mitatu kwa ajili Bi. Nyangoma James ambaye ni mwenye ulemavu, na amefanikiwa kukusanya shilingi 8,750,000/- zikiwemo shilingi 5,000,000/- alizotoa yeye mwenyewe.

Rais Dkt. John Magufuli akiongea na wananchi eneo la Ubungo


Rais Magufuli akimkabidhi Nyangoma James ambaye ni mlemavu wa miguu kitita cha shilingi 

milioni 5 alizomchangia ili apate kununua pikipiki ya miguu mitatu.


Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mama mwenye ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha shilingi  milioni 5. Kushoto aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makore.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.