RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli amelitaja Jiji la Dodoma kuwa ndiyo Halmashauri inayoongoza Nchini kwa ukusanyaji wa kodi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya ndani vilivyopo Jijini humo.
Rais Magufuli iliyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja vilivyopo katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma kwa Mabalozi na Mashirika ya Kimataifa Julai 30, 2018 iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi
Alisema Jiji la Dodoma limekusanya Shilingi Bilioni 24.2 katika mwaka wa fedha 2017/2018, kutokana na mpango wao wa kukusanya Bilioni 19, ambapo Halmashauri nyingine zote Nchini hazikuweza kukusanya kiasi kama hicho, huku akimwagia sifa Mkurugenzi wa Jiji hilo Godwin Kunambi kwa uongozi thabiti.
“Ukikusanya Majiji sita, Halmashauri za Wilaya 137, Mamlaka za Miji 22, na Halmashauri za Manispaa 21, katika hawa wote Dodoma Jiji ndiyo inayoongoza kwa ‘collection’, Tanzania nzima” alisisitiza Rais Magufuli.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi
Katika hafla hiyo, jumla ya hati za umiliki wa viwanja 67 vyenye ukubwa wa ekari tano vilivyopimwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma zilitolewa bure kwa Mabalozi wa Nchi mbalimbali waliopo Tanzania na Mashirika ya Kimataifa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.