Kwa Msaada wa Mtandao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo 2 Mei, 2018 amewasilisha mchango wake wa Tzs 10,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Veyula iliopo Jijini Dodoma ikiwa ni ahadi aliyoitoa kwa wananchi wakati aliposimama kuwasalimia akitokea katika hafla ya ufunguzi wa barabara ya Dodoma hadi Babati.
Mchango huo umewasilishwa na Mhe. Deogratious Njedembi ambaye pia amechangia Tzs 1,000,000 kutimiza ahadi yake na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuanza kuchimba msingi wa ujenzi wa madarasa na kutumia fursa hiyo kuwataka watendaji wote kusimamia zoezi la ujenzi kwa ufanisi na kumwagiza Lt Col Matina Mkuu wa kikosi cha JKT Makutupora kusimamia ukamilishwaji wa madarasa hayo ndani ya wiki tatu.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde na Mkuu wa Wilaya Ndejembi waliungana na wananchi katika zoezi la uchimbaji msingi na baadaye Mhe. Mavunde alikabidhi kiasi cha Tzs 5,000,000, mifuko ya saruji 100 na kuahidi kuongeza Tzs 5,000,000 ya ziada mapema wiki ijayo ikiwa ni mchango kutoka kwa marafiki wa Mbunge huyo, na pia alitumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Rais kwa kusaidia ujenzi wa madarasa hayo.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndugu Godwin Kunambi amewahakikishia wananchi kwamba Halmashauri ya Jiji la Dodoma italipia vifaa na gharama zote za kupaua madarasa hayo ikiwa ni sehemu ya mchango wa Jiji.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Deogratius Ndejembi akimkabidhi Mhe. Mbunge Anthony
Mavunde kiasi cha shilingi 10,000,000 (Milioni Kumi) zilizoahidiwa na Mhe. Rais Dkt.
John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Veyula.
Mhe. Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde (Kushoto) akimkabidhi Mhe. Mkuu
wa Wilaya Deogratius Ndejembi mifuko 100 ya saruji. Katikati ni Mkurugenzi wa Jiji
ndugu Godwin Kunambi na kulia ni Mhe. Diwani wa kata ya Makutupora Elia Lenjila.
Mhe. Mkuu wa Wilaya Deogratius Ndejembi akishiriki pamoja na wananchi kwenye
zoezi la uchimbaji msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Mhe. Mbunge Anthony Mavunde akishirikiana na wananchi wa Jimbo lake la Dodoma
Mjini kata ya Makutupora kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Shule
ya Msingi Veyula.
Wananchi pamoja na viongozi wa Wilaya ya Dodoma Mjini wakishiriki kwenye zoezi
la uchimbaji msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais
Magufuli kuchangia katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.