• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais mpya wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu aapishwa

Imewekwa tarehe: March 19th, 2021

ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Machi, 2021 ameapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hafla ya kuapishwa kwake imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo pia amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mhe. Rais Samia ameshika wadhifa huo baada ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufariki dunia tarehe 17 Machi, 2021 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kula kiapo, Mhe. Rais Samia ametoa salamu za pole kwa Mjane wa Marehemu Mama Janeth Magufuli, Mama wa Marehemu Mama Suzan Magufuli, wanafamilia na Watanzania wote kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Aidha, Mhe. Rais Samia amesema Mhe. Dkt. Magufuli alikuwa na kiu, nia na dhamira ya dhati ya kutaka kuibadili Tanzania kwa mafanikio Zaidi na kwamba Watanzania wote ni mashahidi kwa namna alivyofanikiwa kuibadili taswila ya nchi kwa utendaji wake imara usiotikisika huku akimtanguliza Mungu.

“Sote tulisikia matamanio na maono yake makubwa kwa nchi hii aliyoyatafsiri katika Mipango mikakati na ujenzi wa miradi mikubwa, mimi nilipata bahati ya kuwa makamu wake, alikuwa ni kiongozi asiyechoka kufundisha, kuelekeza kwa vitendo vile anataka nchi iwe au nini kifanyike, amenifundisha mengi, amenilea na kuniandaa vya kutosha, naweza kusema bila chembe ya shaka kuwa tumepoteza kiongozi shupavu, Madhubuti, mzalendo, mwenye maono, mpenda maendeleo, mwamamwema wa Bara la Afrika na mwamamapinduzi wa kweli” amesema Mhe. Rais Samia.

Amewataka Watanzani wote kujenga umoja na mshikamano katika kipindi hiki kigumu na amewahakikishia kuwa Taifa lipo imara na viongozi wamejipanga vizuri kuendeleza pale alipoishia Mhe.  Dkt. Magufuli.

Vilevile, Mhe. Rais Samia ametangaza siku 21 za maombolezo ya Kitaifa ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti na amesisitiza kuwa “Katika kipindi hiki cha maombolezo, huu ni wakati wa kuzika tofauti zetu na kuwa wamoja kama Taifa, ni wakati wa kufarijiana, kuoneshana upendo, udugu wetu, huu sio wakati wa kutazama mbele kwa mashaka bali ni wakati wa kutazama mbele kwa matumaini na kujiamini, si wakati wa kutazama yaliyopita bali kutazama yajayo, sio wakati wa kunyoosheana  vidole  bali ni wakati wa kushikana mikono na kusonga mbele, ni wakati wa kufutana machozi na kufarijiana ili tuweke nguvu zetu za pamoja kujenga Tanzania mpya ambayo mpendwa wetu Rais Magufuli aliitamani”.

Akimalizia, Mhe. Rais Samia amesema mwili wa Dkt. John Pombe Magufuli utazikwa tarehe 25 Machi, 2021 nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.


Chanzo: Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU  Dar es Salaam 19 Machi, 2021










Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.