RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete ameiasa jamii kuona umuhimu wa kuwatunza na kuwathamini wazazi wao katika kipindi cha uhai wao.
Kikwete aliyasema hayo wakati akitoa salaam za rambirambi wakati wa ibada ya kuaga mwili wa mama mzazi wa Wakili Methusela Gwajima, mume wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima nyumbani kwa Wakili huyo mkoani Dar Es Salaam.
Alimpongeza Waziri Dkt. Gwajima na mume wake Wakili Gwajima kwa kuwajali wazazi wao kipindi chote cha uhai wao hadi walipofariki ambapo, mwaka 2019 alifariki Baba mzazi wa Wakili huyo Mzee Stiven Gwajima na mwaka huu amefariki mke wa marehemu Bi. Sophia Gwajima.
Viongozi waliodhuhuria ni pamoja na Shekh Mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis na Waziri Mstaafu wa Maendeleo ya Jamii Mhe. Sophia Simba .
Wengine ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sylivesta Kainda , Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kigamboni na Katibu wa Kamati ya Wanawake Taifa ya Kupinga Ukatili Lilian Wassira, Mwenyekiti wa Taifa wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Fatma Kange, viongozi mbalimbali wa taasisi za Serikali na binafsi, viongozi wa Serikali ya Mtaa, viongozi wa Machinga, Wajane, SMAUJATA , SAWATA, FAGDI na Mtandao wa Malezi.
Mwili wa mama wa Wakili Gwajima Marehemu Sophia Gwajima umesafirishwa kuelekea nyumbani Kisesa, Mwanza ambapo utazikwa Machi 30, 2024.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.