• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Mwinyi mgeni rasmi uwashwaji Mwenge wa Uhuru

Imewekwa tarehe: May 17th, 2021

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo kitaifa zitazinduliwa Uwanja wa Mwehe – Makunduchi, Mkoani Kusini Unguja, Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokutana na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021..

Mheshimiwa Mhagama alisema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2021 ni Mbio maalum, umaalum wake pia unatokana na mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika Wilaya 150 za kiutawala tu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya Halmashauri za Wilaya 195 kama ilivyozoeleka.

“Chombo hiki sasa hakina budi kikimbizwe tena nchini kote baada ya kutofanya kazi toka mwaka 2020 kutokana changamoto za ugonjwa wa Korona, hivyo ili kiweze kurejesha matumaini kwa watanzania na kuwahimiza kuchapa kazi chini uongozi shupavu wa Serikali ya awamu ya sita inayoongwa na Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mhagama

Alifafanua kuwa, falsafa ya Mwenge Mwenge wa Uhuru ndio chimbuko la Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Mwaka 1964 na Azimio la Arusha la mwaka 1967.

Akinukuu maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa mwaka 1958 wakati akihutubia kikao cha 35 cha Umoja wa Mataifa na kuyarudia tarehe 22 Oktoba, 1959 wakati akihutubia Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika (LEGCO) “Sisi watu wa Tanganyika, tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pamejaa chuki na heshima palipo na dharau”

“Ni mwaka wa 29 sasa toka Mbio za Mwenge wa Uhuru zilivyoanzishwa na waasisi wetu na umeendelea kuwa chombo muhimu kwa Taifa kwa kujenga undugu, umoja, mshikamano na kudumisha amani pote unapopita bila kujali itikadi zetu za kisiasa, dini wala makabila yetu.” alieleza

 

Aliongeza kuwa Mwenge wa uhuru na mbio zake zimekuwa na faida kwa taifa ikiwemo kuendelea kuhamasisha Wananchi kushirikiana na Serikali yao katika kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali za maendeleo katika nyanja za kilimo, ufugaji, Uvuvi endelevu, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, umeme na huduma za jamii katika maeneo yote nchini na hasa katika maeneo yasiyofikika kiurahisi.

Pia Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuelimisha wananchi katika maeneo yote nchini jinsi ya kupambana na maradhi yanayotishia ustawi wa watu wetu kama vile UKIMWI, Malaria na kuhamasisha wananchi kushiriki vita dhidhi ya Rushwa na matumizi ya Dawa za kulevya na sasa zitaichukua dhana ya Lishe bora kwa afya Imara ya Watanzania. Pamoja na njia nyingine tunazotumia kuwahamasisha wananchi wetu. Bado Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa ni njia sahihi ya kufikisha taarifa na elimu sahihi ya changomoto zinazowakabili watanzania wote.

Aidha, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wote wa Zanzibar, kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mwehe   Zanzibar na kuungana na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kufanikisha shughuli muhimu kitaifa.

Kwa Upande wake, Kaimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Leila Mohamed Mussa alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamefanikiwa kukamilisha maandalizi kwa asilimia 100.

“Watendaji wa Serikali zote mbili wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ufanisi wa uzinduzi hu una hivyo Mwenge huo kuanza kukimbizwa rasmi” alisema Mheshimiwa Leila

Alitumia pia fursa hiyo kuwaalika wakazi wa Makunduchi na maeneo mengine mbalimbali kujitokeza kwa wingi.

Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2021, unahusu matumizi sahisi ya TEHAMA, chini ya Kauli mbiu isemayo: “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu .Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”. Pamoja na Ujumbe huo, Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi na Viongozi kote nchini, kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, ugonjwa Malaria, mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za Kulevya, Mapambano dhidi ya Rushwa na kuhamasisha Wananchi juu ya Lishe bora kwa afya imara.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.