RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mhe. Rais Samia amesema hayo leo tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya kuwaapisha viongozi hao katika hafal afupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Amesema uteuzi wa viogonzi hao utaleta uwajibikaji mzuri hasa katika sekta ya Habari na Mawasiliano kwa sababu hivi sasa inakwenda kwenye mabadiliko ya kukuza matumizi ya teknolojia na kuwataka viongozi hao kuwajibika katika nafasi zao hizo ili Tanzania ifige hatua kimaendeleo.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka viongozi mbalimbali walioteuliwa akitolea mfano Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kuacha mara moja mivutano isiyo na tija katika majukumu yao.
Naye Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amempongeza Mhe. Rais Samia kwa jitihada zake anazozifanya katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta ya michezo ambayo hivi sasa inafanya vizuri ndani na nje ya nchi.
Akizungumzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali haina wasiwasi nayo kwa sababu watendaji wa Tume hiyo wnatekeleza majukumu yao ipasavyo.
Aidha, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Akson, amewataka viongozi wa Tume ya Uchaguzi kuwa na utaratibu wakufanya matayarisho ya uchaguzi mapemba, badala ya kusubiri hadi uchaguzi unapofika ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wanasiasa dhidi ya Tume hiyo.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amewaongoza viongozi mbalimbali kumuaga Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu hapa nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.