WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha shilingi bilioni 150 kutumika kwa ajili ya ruzuku ya mbolea ili kuwezesha upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa wingi na kwa gharama nafuu.
Mheshimiwa Majaliwa amesema katika msimu wa 2022/2023, utoaji wa ruzuku ya mbolea kwa wakulima unalenga kuongeza uzalishaji wa chakula nchini na hivyo kuwa na usalama wa chakula na kukidhi upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Septemba 23, 2022) wakati akiahirisha mkutano wa nane wa Bunge la 12, Bungeni jijini Dodoma. Amesema Mheshimiwa Rais Samia anatambua umuhimu wa pembejeo katika kuongeza tija kwenye kilimo.
Amesema hadi kufikia tarehe 31 Agosti, 2022 wakulima 956,920 wamesajiliwa kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku ambapo jumla ya tani 60,882 za mbolea zimenunuliwa na wakulima katika mikoa ya Arusha, Iringa, Mbeya, Morogoro, Njombe, Rukwa, Ruvuma na Songwe. “Nitumie fursa hii kuilekeza Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.