RAIS wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa Burundi kwa kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo huku wakiendelea kudumisha amani.
Pia, Mheshimiwa Rais Samia amempongeza Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye kwa jitihada zake za kukuza amani, demokrasia na uchumi.
Hayo yamesemwa leo tarehe Alhamisi, Julai Mosi 2021 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipowasilisha salam za Rais Samia katika sherehe za maadhimisho hayo Jijini Bujumbura.
"Nipo mbele yako nikimuwakilisha Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia. Rais amenituma nilete salamu zake kwako kwamba anawapongeza sana wana-Burundi kwa kuendelea kukuunga mkono" amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Samia amemuhakikishia Rais wa Burundi kwamba ataendeleza uhusiano wa kindugu na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili na pia ameahidi kuitembelea Burundi.
Kwa upande wake, Rais wa Burundi Mheshimiwa Ndayishimiye ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Wana-Burundi waendelee kushikamana na kushirikiana katika kuboresha maendeleo ya nchi yao. "Burundi itajengwa na Warundi wenyewe." Amesisitiza Rais huyo.
Amesema kwa sasa wanajivunia hali ya amani na utulivu uliopo Burundi, hivyo amewataka wananchi wa nchi hiyo waendelee kushikamana na wasikubali kulisaliti Taifa lao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.