RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 29 Septemba, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Mhe. Tony Blair ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change) amemshukuru na kumhakikishia Mhe. Rais Samia kuwa taasisi yake inaunga mkono jitihada mbalimbali anazochukua katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.
Amesema ili kuwa na mafanikio ya haraka katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni muhimu kuwa na taarifa sahihi ambazo zitawezesha ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Mhe. Tony Blair kwa kukutana nae na kumjulisha ufuatiliaji na uratibu wa masuala yanayofanywa na taasisi yake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania. Aidha, amesema kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa vipaumbele vyake kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.