RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philiph Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jina la Dkt. Mpango limesomwa bungeni jijini Dodoma leo Machi 30, 2021 na Spika Job Ndugai aliyeletewa bahasha yenye jina hilo na mpambe wa kiongozi huyo mkuu wa nchi.
Spika Ndugai alianza kusoma nyaraka hiyo ya Mhe. Rais akirudia rudia maneno ya utangulizi kabla ya kulisoma jina ambapo baada ya kusoma jina wabunge walishangilia kwa nguvu.
Wakati hayo yakiendelea Dkt. Mpango alionekana kushikwa na butwaa huku wabunge wakinyanyuka kwenye viti vyao na kumfuata kumpongeza kisha Dkt. Mpango akasimama kuzungumza akishukuru kwa pendekezo hilo huku akielezea pia historia yake.
Baada ya hatua hiyo, Bunge lilianza mchakato wa kuthibitisha jina hilo ambapo Wabunge walimthibitisha kwa asilimia 100 ya kura za Wabunge wote 363.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.